1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simu za mkononi zapunguza idadi ya mbegu za kiume

8 Novemba 2023

Watafiti wamegundua uhusiano kati ya matumizi ya simu za mkononi na kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume za uzazi kwa vijana. Je, unapaswa kuhofii? Soma zaidi

https://p.dw.com/p/4YYCn
Erstes Apple iPhone | im Jahr 2007
Picha: Manuel Balce Ceneta/AP Photo/picture alliance

Kiwango cha mbegu za kiume ulimwenguni kimekuwa kikipungua kwa miongo kadhaa sasa, na ijapokuwa watalaamu wana sababu nyingi wanazohisi zinachangia hali hiyo, hakuna anayejua hasa ni kwa nini hali iko hivyo.

Katika utafiti mpya kutoka Uswisi huenda ukaongeza kwenye orodha hiyo sababu nyingine inayochangia kuwa ni simu za mkononi.

Baada ya kuufanyia utafitisampuli za mbegu za kiume za Zaidi ya vijana 2,800, watafiti wa Uswisi walipata uhusiano kati ya matumizi ya juu ya simu za mkononi na kiwango cha chini cha mbegu za kiume. Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la Uzazi na Utasa.

Hawakupata tofauti katika uwezo wa kusafiri mbegu za kiume kwenye uke au muundo kati ya aina tofauti ya watumiaji wa simu.

Soma pia:Uganda: Ruksa wasichana wadogo kutumia uzazi wa mpango

Pia hawakupata Ushahidi wowote unaoonyesha kuwa kuiweka simu mfukoni, badala ya begi la mgongoni, kwa mfano, kunachangia katika ukolezi wa mbegu za kiume.

Watafiti hao walifanya uchunguzi huo kutoka mwaka wa 2005 hadi 2018. Walipata kuwa uhusiano kati ya matumizi makubwa ya simu na kiwango cha chini cha mbegu za kiume ulionekana wazi zaidi katika miaka ya mwanzo ya utafiti huo kuliko mwishoni.

"muundo huo unatokana na mabadiliko ya teknolojia mji, hasa kutoka mitandao ya 2G hadi 3G na 4G, na kupungua kwa nguvu za simu.

Bado hakuna maelezo ya biolojia yaliyofanywa

Utafiti huu unaongeza simu za mkonono kwenye orodha ndefu ya sababu ambazo watafiti wengine waligundua kuwa huenda zikaharibu uzazi.

Mfano kuvuta sigara, shinikizo la kisaikolojia, pombe, kunenepa kupita kiasi, na kemikali zinazopatikana kwenye sumu za kuwauwa wadudu na mifuko ya plastiki inayofungia mboga tunazonunua madukani.

Mchakato wa utungishaji mimba kwa wanawake- IVF

Profesa Allan Pacy wa afya ya wanaume kutoka Chuo Kikuu cha Manchester na ambaye hakuhusika katika utafiti huo, anasema utafiti huo sio kamilifu, na watayarishaji wa ripoti hiyo wanakiri hilo, lakini ni utafiti katika ulimwengu halisi,  na kwa maoni yake hicho ni kitu kizuri.

Alison Campbell, Mwanasayansi Mkuu wa Care Fertility, ameuita utafiti huo kuwa "wa kufurahisha na ambao haujawahi kuonekana”. Hakushiriki katika utafiti huo.

Hata hivyo Bibi Campbell alisema huenda kukawa na maelezo mengine ya kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume miongoni mwa watumiaji wa mara kwa mara wa simu za mkononi.

Soma pia:Japan yalenga kuimarisha viwango vya uzazi

Pacey anaunga mkono wasiwasi huo. "Hatuwezi kuwa na uhakika kuwa simu ya mkononi sio ishara mbadala kwa kipengele kingine cha mtindo wa wanaume au taaluma yao,"

Aliongeza kwamba hiyo ndio  sababu halisi ya mabadiliko yoyote kwa ubora wa mbegu  za kiume.

 "Kwa sasa hakuna maelezo yaliyothibitishwa ya biolojia au mifumo inayotokana na uchunguzi huu, kwa sababu utafiti bado haujafanyika," alisema.

Wanaume wanapaswa kufanya nini?

Kama wewe ni mwanaume unayepanga kuwa na Watoto wakati mmoja, Habari hizi huenda zikakupa wasiwasi, lakini watafiti wanasema usiwe na hofu wala kufanya mabadiliko makubwa kwa sasa.

Mwanaume akitumia simu ya mkononi kuwasiliana
Mwanaume akitumia simu ya mkononi kuwasilianaPicha: Rodger Bosch/AFP/Getty Images

"kama wanaume wana wasiwasi, basi kuweka simu zao mkobanina kupunguza matumizi ya simu ni kitu rahisi cha wao kufanya,” anasema Pacy.

Soma pia:Mpango wa uzazi kwa njia ya homoni huongeza hatari ya saratani ya matiti

Lakini kwa sasa hakuna Ushahidi kuwa hiyo itaongeza ubora wa mbegu zao za kiume.

"Kwangu mimi, nitaendelea kuiweka simu yangu kwenye mfuko wangu wa suruali.” Alisema huku akiweka simu yake kwenye mfuko wa suruali.