1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Mpango wa uzazi huongeza hatari ya saratani

John Juma
22 Machi 2023

Utafiti wa kiafya umeonyesha kuwa vidhibiti mimba vyote vya homoni vinazidisha kwa kiwango kidogo hatari ya saratani ya matiti.

https://p.dw.com/p/4P5Vp
Contraceptive Pill study
Picha: Tim Ireland/empics/picture alliance

Kulingana na utafiti huo uliotolewa Jumatatu, vidhibiti hivyo ni pamoja na tembe maarufu za progestogeni.

Watafiti walioshiriki kwenye uchunguzi huo wamesisitiza kuwa hatari ya kuongezeka kwa saratani ya matiti inapaswa kupimwa kwa kuzingatia faida za njia hizo za homoni kwa kupanga uzazi, pamoja na kinga za njia hizo dhidi ya aina nyingine za saratani kwa wanawake.

Kulingana na utafiti huo, wanawake wanaotumia njia za homoni kupanga uzazi wana hatari ya kati ya asilimia 20 hadi 30 ya kupata saratani ya matiti, kuliko wale wasiotumia njia za homoni.