1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJapan

Japan yalenga kuimarisha viwango vya uzazi

Saumu Mwasimba
13 Juni 2023

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida anajiandaa leo kuzinduwa mpango maalum wenye lengo la kuleta mageuzi katika viwango vya uzazi vinavyopungua nchini humo.

https://p.dw.com/p/4SVMJ
Watoto wakiwa wanakwenda shuleni kuanza mwaka mpya wa shule nchini Japan.
Chini ya mkakati huo wa waziri mkuu, familia zenye watoto zitaongezewa malipo.Picha: Julian Ryall/DW

Chini ya mpango huo Kishida anataka kuongeza kiwango cha malipo kwa familia zenye watoto. Tangazo hilo la sera ya waziri mkuu Kishida limekuja wakati kukiweko eti eti kwamba kiongozi huyo atalivunja bunge wiki hii na kuitisha uchaguzi wa mapema,hatua ambayo huenda ikazidisha miito kuhusu ongezeko la matumizi kutoka ndani ya chama chake.

Kimsingi uchaguzi wa bunge nchini Japan ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2025 lakini waziri mkuu Kishida aliyetwaa madaraka mwaka 2021 anataka kuimarisha nafasi yake madarakani ndani ya chama kuelekea kinyang'anyiro cha uongozi wa chama hicho mwezi Septemba.