1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yajiondoa katika majaribio ya silaha za nyuklia

2 Novemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini sheria inayoondoa uidhinishaji wa Urusi wa mkataba wa dunia unaopinga majaribio ya silaha za nyuklia.

https://p.dw.com/p/4YKY6
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Gavriil Grigorov/Kremlin Pool/Planet Pix/picture alliance

Hatua hiyo imekosolewa na shirika nalounga mkono ufuataji wa sheria za kudhibiti silaha za nyuklia. Urusi inasema imechukua hatua hiyo ili kuiweka katika kiwango sawa na Marekani ambayo iliusaini mkataba huo ila haikuuidhinisha.

Wanadiplomasia wa Urusi wanasema nchi hiyo haitorudia majaribio ya nyuklia labda tu Marekani ikifanya hivyo.

Wanadiplomasia hao vile vile wanadai hatua hiyo ya Rais Putin haitoubadilisha msimamo wake wa nyuklia licha ya kuwa na hifadhi kubwa ya silaha za nyuklia duniani au jinsi itakavyotoa taarifa kuhusiana na harakati zake za nyuklia.

Putin aitisha mkutano kufuatia uvamizi wa uwanja wa ndege

Hatua hiyo ni ushahidi wa uhasama uliopo kati ya Marekani na Urusi ambao mahusiano yao yako katika kiwango cha chini kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1962.