1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto: Mpango wa kutuma askari wa Kenya, Haiti unaendelea

30 Januari 2024

Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali yake itaendelea na mipango ya kuongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa kurejesha utulivu nchini Haiti licha ya mahakama mjini Nairobi kuzuia.

https://p.dw.com/p/4bqiZ
Nairobi, Kenya | Rais Willium Ruto
Rais wa Kenya Willium RutoPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Kikosi hicho cha kimataifa kinanuiwa kwenda kukabiliana na vurugu za magenge ya wahumi na wabeba silaha ambayo yameuteteresha usalama wa Haiti ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya karibu watu 5,000. 

Hatma ya ujumbe huo iliingia mashakani baada ya mahakama ya mji wa Nairobi kutoa uamuzi kuwa upelekeaji askari wa Kenya nchini Haitiitakuwa kinyume na katiba isipokuwa kama kutakuwa na makubaliano na serikali ya nchi hiyo.

Soma pia:Serikali ya Kenya yaapa kupinga uamuzi wa mahakama dhidi ya kupeleka maafisa wa polisi nchini Haiti

Kwenye mahojiano na shirika la habari la Reuters, rais Ruto amesema mipango tayari itaelendelea ya kutumia pendekezo hilo la mahakama la kuwepo mkataba wa nchi mbili kuwezesha ujumbe huo wa kulinda amani kutumwa nchini Haiti.

Amesema tayari Haiti ilituma maombi rasmi kwa serikali ya Kenya na mipango inafanyika kutuma polisi nchini humo.