1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kenya yaizuwia serikali kupeleka askari Haiti

26 Januari 2024

Mahakama nchini Kenya imeizuia serikali kuwapeleka maafisa wa polisi nchini Haiti kuongoza kikosi klichoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kulisaidia taifa hilo la Karibiani kukabiliana na magenge yenye silaha.

https://p.dw.com/p/4bhh3
Haiti I Port-au-Prince
Raia nchini Haiti wakikimbia mapigano ya magenge yenye silaha katika mji mkuu, Port-au-Prince.Picha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita, amesema Kenya inaweza tu kupeleka maafisa wake wa polisi kuhudumu nje ya nchi iwapo kutakuwepo na "mpangilio sawa na huo" na serikali mwenyeji.

Mnamo mwezi Oktoba, upinzani uliupinga uamuzi wa serikali wa kutuma maafisa 1,000 wa polisi ili kushughulikia mzozo unaozidi kuongezeka nchini Haiti, ambapo magenge ya wahalifu yamewalazimisha karibu watu 200,000 kuyakimbia makaazi yao.

Soma zaidi: Waziri wa mambo ya nje wa Haiti asema ghasia nchini humo ni sawa na eneo la vita

Haiti imekabiliwa na ongezeko la ghasia tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moise mnamo mwezi Julai mwaka 2021 katika makaazi yake mjini Port au Prince.