1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres ashitushwa na Israel kutumia akili bandia Gaza

5 Aprili 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake juu ya ripoti kwamba Israel inatumia akili ya kubuni kubaini shabaha ya mashambulizi yake kuelekea Gaza.

https://p.dw.com/p/4eTeY
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameshitushwa na ripoti kwamba Israel inatumia akili bandia kuishambulia Gaza.Picha: Omar Havana/AP/picture alliance

Kauli ya Guterres inajiri baada ya Marekani kusema inafuatilia madai ya ripoti za vyombo vya habari kwamba Israel imekuwa ikitumia akili ya kubuni kuisaidia kuchagua maeneo ya kushambulia.

Soma zaidi: Iran yasisitiza itaiadhibu Israel kwa kushambulia ubalozi

Hata hivyo, msemaji wa Ikulu ya White House, John Kirby, alisema nchi yake bado haikuwa imethibitisha undani wa ripoti ambayo inataja kwamba Israel inatumia mfumo wa akili ya kubuni wenye uangalizi mdogo wa kibinaadamu.

Jeshi la Ulinzi la Israel limekanusha madai hayo.