1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasisitiza itaiadhibu Israel kwa kushambulia ubalozi

5 Aprili 2024

Iran imesisitiza ahadi yake ya kuiadhibu Israel wakati wa mazishi ya maafisa saba waliouawa katika shambulizi la anga linaloshukiwa kufanywa na Israel kwenye kambi ya ubalozi wa Iran nchini Syria mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/4eTcM
Maziko ya majenerali wa Iran waliouawa Syria na jeshi la Israel
Viongozi wa Iran wakiwa kwenye mazishi ya majenerali wa kijeshi waliouawa kwenye mashambulizi ya jeshi la anga la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria.Picha: AP/picture alliance

Televisheni ya taifa ya Iran imeonesha waandamanaji wakiwa wamebeba picha za waliouawa na mabango huku wakipaza sauti za kulaani mauaji hayo.

Soma zaidi: Israel yasema shambulizi lililowauwa wafanyakazi wa misaada lilikuwa "kosa kubwa"

Akihutubia umma huo, Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi (IRGC), alisema watalipiza kisasi.

Siku ya Alkhamis (Aprili 4), Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema nchi yake ingemdhuru "yeyote" anayeidhuru au kupanga kulidhuru taifa lake.