1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Uingereza laridhia kupeleka wakimbizi Rwanda

Mohammed Khelef
13 Desemba 2023

Wabunge nchini Uingereza wamepiga kura ya kuunga mkono mpango wa serikali kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, ambao umekigawa chama tawala cha Conservative, chake Waziri Mkuu Rishi Sunak.

https://p.dw.com/p/4a5nt
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak.Picha: James Manning/REUTERS

Baada ya majadiliano makali, wabunge 313 walipiga kura kuridhia kile kiitwacho "Usalama wa Rwanda", mswaada wa Sheria ya Kuomba Hifadhi na Uhamiaji, huku 269 wakiupinga.

Muswaada huo wa dharura unachukuliwa kamajibu la Sunakkwa uamuzi wa Mahakama ya Juu ambayo mwezi Novemba ilisema kwamba kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ni kinyume na sheria ya kimataifa.

Soma zaidi: Mpango wa Sunak kuwapeleka wakimbizi Rwanda wapata upinzani

Hata hivyo, bado kundi la wabunge wa chama chake wanaopingana na sheria hiyo, limeapa kuja na mapendekezo mapya kwa sheria mwezi ujao wa Januari, hatua inayomuweka Sunak kwenye vita vipya ndani ya Conservative.