1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUlaya

Sunak akabiliwa na upinzani bungeni juu ya sera ya wakimbizi

Amina Mjahid
12 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, anakabiliwa na upinzani bungeni juu ya wadhfa wake wa uwaziri mkuu wakati ambapo wabunge nchini humo leo watapiga kura kuamua juu ya mpango wa kuwahamishia waomba hifadhi Rwanda.

https://p.dw.com/p/4a4Bb
Uingereza | Waziri Mkuu wa Rishi Sunak akiwa bungeni
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, akizungumza bungeni wakati wa maswali na majibuPicha: UK Parliament/Jessica Taylor/REUTERS

Mwezi uliopita Mahakama ya Juu kabisa ya Uingereza ilitoa hukumu kwamba Rwanda sio nchi salama kuwatupeleka watu wanaowasili Uingereza kwa boti kwenye fukwe za kusini mwa kisiwa cha England, na kwamba mpango huo wa serikali ni kinyume cha sheria za Uingereza na za kimataifa. 

Soma pia:Sunak: Tutafanikiwa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Hata hivyo baada ya uamuzi huo, Sunak alifikia makubaliano mapya na Rwanda na amewasilisha bungeni sheria tata inayokiuka sheria za haki za binaadamu za ndani ya nchi yake na za kimataifa. 

Ikiwa wabunge 30 tu wa chama tawala cha Conservative wataungana na upinzani, sheria hiyo iliyokigawa chama hicho haitopita hatua ambayo itakuwa ni pigo kubwa kwa Rishi Sunak.