1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky aapa kulipiza mashambulizi yaliyofanywa na Urusi

Saumu Mwasimba
9 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi ya Urusi hayapaswi kufumbiwa macho bila kujibiwa.

https://p.dw.com/p/4b1Do
Volodymir Zelensky rais wa Ukraine
Volodymir Zelensky rais wa UkrainePicha: AFP/Getty Images

Katika hotuba yake aliyoitowa kwa njia ya video jana jioni, kiongozi huyo wa Ukraine amesema magaidi wanapaswa kulipia gharama ya uharibifu uliosababishwa na kitendo cha ugaidi na Urusi itawajibika.

Watu wanne waliuwawa na wengine 45 walijeruhiwa katika miji ya Kharkiv, Zaporizhzhya na Khmelnytskyi jana Jumatatu.

Zelensky pia amebaini kwamba majadiliano na washirika wa kimataifa wa Ukraine yatakayofanyika wiki kadhaa zijazo yatajikita katika kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi hiyo.

Jana Urusi ilivurumisha mkururo wa maroketi  na makombora pamoja na mashambulizi ya droni dhidi ya Ukraine.