1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelenskiy atoa wito wa silaha zaidi kwa Ukraine

Lilian Mtono
26 Oktoba 2023

Ukraine yataka kujitetea dhidi ya Urusi baada ya majengo katika kinu cha nyuklia cha Kh mel nytskyi kushambuliwa.

https://p.dw.com/p/4Y2XZ
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymir ZelenskyPicha: president.gov.ua

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa wito wa msaada zaidi wa silaha wakati taifa hilo likiendelea kujitetea dhidi ya Urusi baada ya majengo katika kinu cha nyuklia cha Kh mel nytskyi kushambuliwa.

Amesema shambulizi kwenye kinu hicho cha nyuklia kwa mara nyingine linawakumbusha wao na washirika wao juu ya umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa angani.

Zelenskiy amesema hayo katika ujumbe wa video jana jioni na kuongeza kuwa shambulizi hilo linaonyesha namna Urusi inavyoweza kukwepa vikwazo kirahisi kwa kutumia baadhi ya vifaa vya magharibi kwenye droni na makombora yake.

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu 16.