1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroEthiopia

Zaidi ya watu 50,000 wayakimbia makaazi yao Ethiopia

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watu 50,000 wameyakimbia makaazi yao kutokana na mapigano katika eneo linalozozaniwa kaskazini mwa Ethiopia

https://p.dw.com/p/4f5C5
Maelfu waliofimbia makwao wahitaji misaada Ethiopia
Maelfu waliofimbia makwao wahitaji misaada EthiopiaPicha: Ed Ram/Getty Images

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa jana jioni imesema idadi hiyo ya watu ni katika miji ya Alamata, Raya Alamata, Zata na Ofla, tangu Aprili 13.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa hali ya kibinadamu inazidi kuzorota, huku maelfu ya wanawake na watoto wakihitaji msaada mkubwa wa kiutu. Vikosi vya Amhara viliudhibiti mji wa Raya Alamata kusini mwa mji wa Tigray, wakati wa vita vilivyodumu kwa miaka miwili baina ya serikali ya Ethiopia na vikosi vya Tigray.

Chini ya makubaliano ya amani kati ya serikali na mamlaka ya Tigray, vikosi vya Amhara ambavyo viliunga mkono wanajeshi wa shirikisho, vilipaswa kujiondoa kutoka mji wa Raya Alamata baada ya makubaliano hayo kusainiwa huko Pretoria mwaka 2022.