1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 700,000 hatarini kupata utapiamlo hatarini - UNICEF

Iddi Ssessanga
9 Februari 2024

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema watoto 700,000 nchini Sudan wapo hatarini kukumbwa na utapiamlo mbaya zaidi mwaka huu, ambapo huenda makumi kwa melfu kati yao wakapoteza maisha.

https://p.dw.com/p/4cET8
Wakimbizi wa ndani kwenye vita vya Sudan.
Wakimbizi wa ndani kwenye vita vya Sudan.Picha: Michael Kappeler/picture alliance/dpa

Msemaji wa UNICEF, James Elder, alisema bila ya kupata msaada wa ziada shirika hilo halitaweza kuwatibu zaidi ya watoto 300,000 kati ya wale wasiofikiwa vyema, na kwa hivyo makumi ya maelfu huenda wakafa.

Soma zaidi: UNICEF yaomba dola bilioni 9.3 za kusaidia watoto 2024

Elder aliainisha aina mbaya zaidi ya utapiamlo, ambao unamfanya mtoto awe na uwezekano mara kumi wa kufa kutokana na maradhi kama vile kipindupindu na malaria.

Soma zaidi: Mataifa zaidi kuwaondoa raia wao Sudan

Alisema watoto milioni 3.5 wanatazamiwa kukumbwa na utapaiamlo huo mbaya.

Siku ya Alhamis (Februari 8), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, aliayahimiza mataifa kutowasahau raia waliozingirwa katika vita vya Sudan, na kutoa maombi ya dola bilioni 4.1 ili kushughulikia mahitaji yao ya kiutu.