1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

Wakimbizi 15,000 wa Afghanistan waondoka Pakistan

Amina Mjahid
5 Novemba 2023

Serikali ya Pakistan imewarejesha nyumbani wakimbizi 15,000 wa Afghanistan ndani ya saa 24 kufuatia taifa hilo kuanza mchakato wa kuwasaka wahamiaji haramu.

https://p.dw.com/p/4YQJa
Serikali ya Pakistan imewarejesha nyumbani wakimbizi 15,000 wa Afghanistan ndani ya saa 24 kufuatia taifa hilo kuanza mchakato wa kuwasaka wahamiaji haramu
Serikali ya Pakistan imewarejesha nyumbani wakimbizi 15,000 wa Afghanistan ndani ya saa 24 kufuatia taifa hilo kuanza mchakato wa kuwasaka wahamiaji haramuPicha: The Norwegian Refugee Council/REUTERS

Kulingana na takwimu za serikali, takriban wakimbizi milioni 4.4 wa Afghanistan wanaishi Pakistan huku milioni 1.7 kati yao wakikosa vibali halali vya kuwaruhusu kuishi nchini humo.

Mwezi uliopita Pakistan ilitangaza kuwarejesha nyumbani wakimbizi wote wa Aghanistan wanaoishi huko kinyume cha sheria, hatua iliyokosolea na serikali za Magharibi na mashirika ya kutetea haki za binaadamu.

Pakistan ilichukua uamuzi huo baada ya miezi kadhaa ya mvutano na watawala wa Taliban Afghanistan, kufuatia mashambulizi yanayofanyika katika maeneo ya mpakani mwa mataifa hayo mawili. Pakistan inadai mashambulizi hayo yanafanywa na wanamgambo wanaotekeleza operesheni zao kutoka upande wa Afghanistan.

Aidha wachambuzi wanasema hatua ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Afghanistan, imechukuliwa ili kuipa shinikizo Taliban kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo hao.