1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wakimbizi 10,000 wa Afghanistan wakimbilia mpaka wa Pakistan

Bruce Amani
31 Oktoba 2023

Zaidi ya Waafghanistan 10,000 wanaoishi nchini Pakistan wamekimbilia mipakani, masaa machache tu kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa kwa watu milioni 1.7 kuondoka kwa hiari au wakamatwe na kufukuzwa.

https://p.dw.com/p/4YDzY
Pakistan | Migranten aus Afghanistan
Wakimbizi wa Afghanistan wakiwa mpakani mwa Pakistan kurudi makwao.Picha: Sophie Kirby/DW

Zaidi ya Waafghanistan 10,000 wanaoishi nchini Pakistan wamekimbilia mipakani leo, saa chache tu kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa kwa watu milioni 1.7 kuondoka Pakistan kwa hiari au wakamatwe na kufukuzwa nchini.

Serikali ya Pakista imesema itaanza kuwakamata Waafghanistan wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini humo na kuwapeleka kwenye vituo vipya vya kuwashikilia kwa muda kuanzia kesho, ambapo watakaguliwa na kurudishwa Afghanistan kwa nguvu.

Soma zaidi: Mtu mmoja afariki katika tetemeko Afghanistan

Nchini Afghanistan, serikali ya Taliban imeweka sheria kali ya kiislamu tangu ilipokamata madaraka Agosti 2021.

Imewapiga marufuku wasichana dhidi ya kupata elimu ya sekondari na chuo kikuu na kuwalazimisha wanawake kutofanya kazi.

Afisa mwandamizi kwenye mpaka wa Torkham katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa amesema kufikia leo asubuhi kulikuwa na karibu watu 10,000 mpakani hapo.

Amesema idadi hiyo inaendelea kuongezeka.

Nchini Afghanistan, serikali ya Taliban imeitaja sera hiyo ya Pakistan kama "unyanyasaji".