1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waisraeli wanapiga kura

Sudi Mnette
1 Novemba 2022

Waisrael leo hii wanapiga kura kwa mara ya tano ndani ya kipindi cha miaka minne, katika uchaguzi mkuu ambamo waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu anafanya jitihada za kurejea tena katika nafasi yake ya awali.

https://p.dw.com/p/4IupZ
Vor den Wahlen in Israel
Picha: Ilia Yefimovich/dpa/picture alliance

Wachambuzi wanakitathimi kinyang'anyiro hicho kwa kukipa nafasi nzuri chama mrengo wa kulia kuwa kama mtawala katika kile kinachoonekana uwezekano wa serikali ya muungano. Baada ya miaka mingi ya mkwamo wa kisiasa, hasira za wapiga kura zinaweza kuathiri ushiriki wa zoezi hilo.

Lakini uungwaji mkono mkubwa wa kambi ya Uzayuni na mpinzani mwenye msimami mkali, Itamar Ben-Gvir  kumebadilisha mwelekeo wa kampeni.

Israel | Wahlen
Wagombea Yair Lapid, Yesh Atid OrtPicha: Tania Kraemer/DW

Waziri Mkuu aliyedumu kwa muda mrefu zaidi madarani huko Israel, Benjamin Netanyahu anaendelea na mashtaka yanayomkabili mahakamani yanayohusu tuhuma za  rushwa, ambayo anakanusha, lakini chama chake cha Likud bado kinatarajiwa kuhitimisha uchaguzi huu kikiwa na wingi wa wabunge.

Muda mfupi baada ya kupga kura yake mjini Jerusalem, kiongozi huyo wa upinzani alisema ana matumaini kwamba watamaliza siku kwa tabasamu lakini hilo lipo katika uamuzi wa watu wenyewe."Ni wajibu na heshima kubwa kujitokeza kupiga kura. Ni wazi kabisa nasema hili kwa wafuwasi wetu, lakini pia kwa ujumla kwa raia wa Israel. Nakwambia wewe nikiwa na mashaka kidogo, lakini Mungu atasaidia, natumaini tutamaliza siku kwa tabasamu,ingawa ni juu yenu, kila mmoja atafanya uamuzi. Ninachotumai tu, ni kwamba hamtaipuuza haki yenu ya kidemokrasia kupiga kura kwa zingatio la hatma ya nchi"

Kura ya maoni yanenesha Benjamin Netanyahu atakabiliwa na ugumu

Hata hivyo wakati vituo vya kupiga kura vikifunguliwa leo hii, uchunguzi wa maoni wa juma lililopita unaonesha kiongozi huyo wa zamani bado ana upungufu wa viti 61 vinavyohitajika katika kumpa wingi katika bunge la Israel - Knesset, lenye wabunge 120, hatua ambayo inaonesha mashaka ya kuwepo kwa juma zima la matarajio ya mzozo wa kuunda serikali ya muungano na pia uwezekano wa uchaguzi mpya.

Mchakato huu wa upigaji kura unafanyika baada ya kuvunjika kwa kile kilichoitwa muungano wa mabadiliko, ambao uliviunganisha vyama vinane vilivyotofautiana, na kufanikiwa kumuondoa madarakani Netanyahu mwaka uliopita lakini kwa bahati mbaya ulishindwa kufanikisha utulivu wa kisiasa.

Soma zaidi: Israel yataka nguvu za kijeshi kutumika dhidi ya Iran

Waziri Mkuu wa sasa Yair Lapid bado ana nia kudhibiti wadhfa wake wakati chama chake cha Yesh Atid kikonekana kuwa nyuma kidogo ya cha Netanyahu cha mrengo wa kulia Likud katika kura ya maoni. Lapid ambae aliwahi kuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni nae leo pia amesikikia katika kituo cha kupigia kura cha Tel Aviv akiwahimiza wapiga kura kujitokeza vituoni kutimiza wajibu wao.

Vyanzo: AP/AFP/RTR