1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Marekani: Urusi imekuwa ikiwaua wanajeshi waliopuuza maagizo

Lilian Mtono
27 Oktoba 2023

Marekani imesema imepata taarifa kwamba jeshi la Urusi limekuwa likiwaua wanajeshi ambao hawatii maagizo yanayohusiana na vita vyake nchini Ukraine, Ikulu ya White House imesema jana.

https://p.dw.com/p/4Y5Dk
John Kirby katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari katika ikulu ya White House.
John Kirby katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari katika ikulu ya White House.Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Msemaji wa ikulu ya White House John Kirby amesema wana taarifa za makamanda wa Urusi kutishia kuua kikosi kizima ikiwa watarudi nyuma kwa hofu ya mashambulizi ya makombora ya Ukraine akisema huo ni ukatili mkubwa.

Hata hivyo, wawakilishi kutoka ikulu ya Urusi, Kremlin, wizara ya ulinzi na ubalozi wa Urusi nchini Marekani hawakutaka kuzungumzia madai hayo walipoombwa kufanya hivyo.

Marekani imekuwa ikipinga vikali uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ikiungwa mkono na mataifa mengine hususan ya magharibi.