1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Usalama wa chakulaAmerika ya Kaskazini

UNRWA: Hakuna mabadiliko kuhusu misaada inayoingia Gaza

John Juma
16 Aprili 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina UNRWA, limesema leo kwamba hakuna mabadiliko makubwa kuhusu viwango vya misaada vinavyoingia Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4erHh
Israel-Hamas | Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina UNRWA
Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina UNRWAPicha: AFP/Getty Images

Kwenye taarifa yake, shirika hilo limesema katika mwezi huu wa Aprili, malori 181 ya misaada ndiyo yamekuwa yakiingia Gaza kila siku kupitia kivuko cha kati ya Israel na Misri.

Kulingana na shirika hilo, idadi hiyo ni ya chini zaidi ikilinganishwa na jumla ya malori 500 yanayotarajiwa kupeleka misaada Gaza kila siku.

Soma pia:Israel: Mashambulizi ya Iran hayatapoteza lengo letu Gaza

Shambulizi la Oktoba 7 la wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel, lilisababisha vifo vya takriban watu 1,200 na mamia kadhaa kuchukuliwa mateka.

Mashambulizi ya Israel kujibu mashambulizi hayo katika ukanda wa Gaza yamesababisha mauaji ya wapalestina zaidi ya 32,000.

Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya zimeliorodhesha kundi la Hamas kama la kigaidi.