1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko ya tabianchi yawahamisha Watoto milioni 43.1

6 Oktoba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema Alhamisi kuwa mafuriko, dhoruba, ukame na mioto vimepelekea watoto milioni 43.1 kuyahama makazi yao kati ya 2016 na 2021

https://p.dw.com/p/4XBK1
Ron Havivs Fotographie |  UNICEF Foto des Jahres 2022
Picha: Ron Haviv, USA, VII for 1843/Economist/picture alliance

Shirika hilo limeuonya kuwa huu ni mwanzo tu na kusema hayo yinachochewa na ongezeko la joto duniani, ambapo sehemu zilizokumbwa zaidi na kadhia hiyo ni Ufilipino, India, China, Canada na Marekani.

Makadirio ya muda yanaonesha kuwa mafuriko yanayohusishwa na mito kuvunja kingo zake, yanaweza kupelekea  watoto  milioni 96 kuyahama makazi yao katika miaka 30 ijayo. Vimbunga vinakadiriwa kuwa vitawahamisha watoto milioni 10.3 huku dhoruba ikiwahamisha milioni 7.2.