1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu chakula Sahel

11 Januari 2023

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu mzozo mkubwa wa chakula katika eneo la Sahel ambao umekolezwa makali na vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4M0Zy
Äthiopien Tigray Shire | eritreisches Flüchtlingslager
Picha: Joerg Boethling/IMAGO

Watu wengine milioni tano zaidi wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa upatikanaji wa chakula, huku Burkina Faso, Niger na Nigeria zikiwa miongoni mwa nchi zilizoathiriwa sana.

Ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa baraza la usalama la umoja huo jana Jumanne inasema miongoni mwa mambo yanayosababisha mzozo huo ni uhaba wa ngano na mbolea uliotokana na vita vya Ukraine, kukosekana usalama katika ukanda wa Sahel, hasa nchini Burkina Faso na Mali, na ongezeko la athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ripoti hiyo pia imesema hali ya kibinadamu, hususan katikati mwa Sahel, bado ni mbaya na inazidishwa makali na kupanda kwa bei za chakula na nishati, pamoja na majanga yanayohusiana na hali ya hewa, yaliyosababishwa na mvua kubwa, mafuriko na uchafuzi wa maji.