1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu washuhudia joto kali zaidi miezi mitatu iliyopita

Lilian Mtono
6 Septemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia hali ya hewa, limearifu siku ya Jumatano kwamba miezi mitatu iliyopita ilikuwa na joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa duniani.

https://p.dw.com/p/4W097
Joto kali India
Mwanaume akiosha uso wake kwa maji kando ya barabara katika iliyokuwa na joto kali mjini New Delhi mnamo Juni 7, 2023.Picha: ARUN SANKAR/AFP/Getty Images

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia hali ya hewa, limearifu leo kwamba miezi mitatu iliyopita ilikuwa na joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa duniani.

Shirika hilo limearifu hayo likinukuu takwimu za Idara ya Umoja wa Ulaya inayojijihusisha na masuala ya mabadiliko ya tabianchi la Copernicus Climate Change, na kuongeza kuwa mwezi Agosti ulivunja rekodi ya kuwa na joto kali zaidi kwa tofauti kubwa na wa pili kwa kiwango cha juu cha joto baada ya mwezi Julai, 2023.Ulaya yakumbwa na matokeo mabaya ya hali ya hewa

Mwezi huo wa Agosti kulingana na shirika hilo ulipindukia wastani wa karibu nyuzi joto 1.5 za Celsius ikilinganishwa na wakati wa kabla ya mapinduzi ya kiviwanda, huku katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akionya juu ya kitisho dhahiri kitokanacho na mabadiliko ya tabianchi.