1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 150,000 wa Urusi wameuawa katika vita vya Ukraine

Lilian Mtono
3 Mei 2024

Ufaransa inakadiria kuwa wanajeshi 150,000 wa Urusi wameuawa tangu taifa hilo lilipoivamia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4fTBA
Stéphane Séjourné
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Stephane SejournePicha: JOSEPH EID/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Stephane Sejourne, amesema hayo kwenye mahojiano na gazeti la Urusi la Novaya Gazeta Europe yaliyochapishwa hii leo na kuongeza kuwa Paris inakadiria majeruhi kufikia 500,000.

Hata hivyo, Urusi haijachapisha taarifa zozote za uharibifu uliotokea katika vita hivyo vilivyoingia mwaka wa tatu.

Urusi yatangaza imelidhibiti kikamilifu eneo la Berdychi

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alisema mwezi Februari kwamba wanajeshi 180,000 wa Urusi waliuawa, huku Uingereza ikisema karibu wanajeshi 450,000 wameuawa kwenye vita hivyo.