1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akimbilia Mahakamani kuzuwia asiondolewe kwenye kura

Bruce Amani
8 Februari 2024

Mawakili wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, wamefunguwa shauri kwenye Mahakama ya Juu kutaka mteja wao asiondolewe kwenye karatasi ya kura kutokana na matukio yanayohusiana na uvamizi wa bunge mwaka 2021.

https://p.dw.com/p/4cBdd
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, anapigania kusalia kwenye karatasi ya kura.
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, anapigania kusalia kwenye karatasi ya kura.Picha: Charly Triballeau/AFP/Getty Images

Majaji tisa, wakiwemo watatu aliowateuwa Trump wakati akiwa rais, watasikiliza hoja za kuukatia rufaa uamuzi uliotolewa na mahakama ya ngazi ya chini uliomuondosha rais huyo wa zamani kwenye kura za mchujo za chama cha Republican katika jimbo la Colorado.

Mabadiliko ya 14 ya katiba ya Marekani yanamzuwia mtu yeyote aliyeshiriki uasi kushikilia ofisi ya umma.

Lakini kwa mujibu wa wanasheria wake, katiba ya nchi hiyo inamlinda rais aliyepo madarakani dhidi ya mashitaka na kwamba hakuhusika na tukio la uvamizi wa bunge mwezi Januari 2021, ambapo wafuasi wake walitaka kuzuwia bunge hilo kuidhinisha matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi hasimu wake, Joe Biden.