1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier: Ujerumani imefikia ukomo wa kupokea wahamiaji

Lilian Mtono
20 Septemba 2023

Rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-walter Steinmeier amekiri hii leo kwamba taifa hilo kwa sasa kukabiliwa na changamoto ya kupokea wahamiaji zaidi.

https://p.dw.com/p/4WblZ
Rais Steinmeier aidha amekiri kwamba Italia pamoja na Ujerumani wamebeba mzigo mzito na kutoa mwito wa mgawo sawa wa mzigo huo wa wahamiaji ndani ya Ulaya.
Rais Steinmeier aidha amekiri kwamba Italia pamoja na Ujerumani wamebeba mzigo mzito na kutoa mwito wa mgawo sawa wa mzigo huo wa wahamiaji ndani ya Ulaya.Picha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Rais Steinmeier amesema kwenye mahojiano na gazeti la Italia la Corriere della Sera kwamba Ujerumani pia imefikia ukomo wa uwezo wa kupokea wahamiaji na kuongeza kuwa taifa hilo limepokea theluthi ya waomba hifadhi wote kwenye Umoja wa Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

Rais huyo aidha amekiri kwamba Italia pamoja na Ujerumani wamebeba mzigo mzito na kutoa mwito wa mgawo sawa wa mzigo huo wa wahamiaji ndani ya Ulaya.

Rais Steinmeier amesema hayo wakati akianza ziara ya siku tatu nchini Italia ambako amekutana na rais Sergio Mattarella pamoja na kutembelea kisiwa cha Sicily, kusini mwa taifa hilo.