1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Kipindupindu kiliongezeka mwaka 2022

Lilian Mtono
25 Septemba 2023

Ripoti ya shirika la afya ulimwenguni, WHO imesema idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kote ulimwenguni iliongezeka mara mbili mwaka uliopita wa 2022.

https://p.dw.com/p/4WkyI
Syria ni moja ya nchi zilizoathirika pakubwa na kipindupindu kutokana na mizozo na uhaba wa maji kama mtoto huyu wa nchini humo anavyoonekana akichota maji machafu kwa matumizi mbalimbali
Syria ni moja ya nchi zilizoathirika pakubwa na kipindupindu kutokana na mizozo na uhaba wa maji kama mtoto huyu wa nchini humo anavyoonekana akichota maji machafu kwa matumizi mbalimbaliPicha: Rami Alsayed/NurPhoto/picture alliance

Shirika la WHO limesema jana Jumapili kwamba, visa 470,000 viliripotiwa mwaka wa 2022 ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na visa 220,000 vya mwaka uliopita.

Hata hivyo wataalam wa WHO wanaamini kuwa takwimu hizo bado hazijitoshelezi na katika makadirio ya awali, lilitabiri kuwepo wagonjwa milioni 1.3 hadi 4 na vifo va hadi watu 143,000 kila mwaka.

Afghanistan, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Nigeria, Somalia na Syria ziliathirika zaidi katika mwaka ulioshuhudia mlipuko wa juu zaidi ya ugonjwa huo.

Milipuko ya kipindupindu inahusishwa zaidi na uhaba wa maji ya kunywa mahitaji, umaskini na migogoro, na kadiri mlipuko unavyoongezeka, ndivyo inavyozidi kuwa ngumu kudhibitiwa