1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal huenda ikazifunga kambi za jeshi la Ufaransa

17 Mei 2024

Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko ametaja uwezekano wa kufunga kambi za jeshi la Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4fxtg
Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko
Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko Picha: Sylvain Cherkaoui/AP/dpa

Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko ametaja uwezekano wa kufunga kambi za jeshi la Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Sonko ameyasema hayo wakati ya hotuba yake ambayo ilizungumzia kuhusu sarafu ya CFA, mikataba ya mafuta na gesi pamoja na haki za mashoga.

Soma: Rais Faye amteua Sonko kama Waziri Mkuu wa Senegal

Sonko amehoji ni kwanini ziadi ya miaka 60 baada ya Uhuru, Ufaransa bado ina wanajeshi karibu 350 nchini humo na kuwataka raia wa Senegal kutathmini faida na athari za hatua hiyo. Amezitaka pia nchi za Magharibi kutoshinikiza mabadiliko ya kijamii na kitamaduni.Senegal yaitaka Ujerumani kubakisha majeshi yake Mali

Sonko amesema ushoga umekuwepo siku zote nchini Senegal lakini kama ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika, hawewezi kuhalalisha jambo hilo.

Sonko ameyasema hayo jana jioni mjini Dakar katika mkutano wa pamoja na mwanasiasa wa Ufaransa wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon, na kusisitiza kuwa atadumisha mahusiano na mataifa ya Mali, Burkina Faso na Niger ambayo pia yaliamua kuwafurusha wanajeshi wa Ufaransa.