1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Saudi Arabia na Qatar waikosoa miito ya Israel kuhusu Wagaza

Josephat Charo
4 Januari 2024

Saudi Arabia na Qatar zimelaani vikali kauli za mawaziri wawili wa Israel kutaka Wapalestina wahame kutoka Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4arsH
Nchi kadhaa zalaami mpango wa Israel wa kuwahamisha wakaazi wa Gaza
Nchi kadhaa zalaami mpango wa Israel wa kuwahamisha wakaazi wa GazaPicha: Mohammed Ali/Xinhua/picture alliance

Waziri wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben-Gvir siku ya Jumatatu alitoa wito wa kuendeleza suluhisho la kuwahimiza wakazi wa Gaza wahame na kuanzishwa tena kwa makazi ya Israeli katika Ukanda wa Gaza, siku moja baada ya Waziri wa Fedha mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich kutoa matamshi kama hayo.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Saudia imesema Saudi Arabia inalaani na kukataa matamshi ya mawaziri hao wawili. Marekani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya pia wameshutumu kauli hizo.