1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Lula atoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa Haiti

29 Februari 2024

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ameitaka dunia kuishughulikia Haiti kwa haraka.

https://p.dw.com/p/4d0EU
Addis Ababa Ethiopia | Mkutano wa AU | Rais Lula wa Brazil
Rais wa Brazil Luiz Lula da SilvaPicha: REUTERS

Lula ameyasema haya katika mkutano wa kilele wa mataifa ya Caribbean ambapo kulifikiwa makubaliano ya kisiasa kuhusiana na nchi hiyo iliyo kwenye mgogoro.

Rais huyo wa Brazil amesema hatua za haraka zinastahili kuchukuliwa ili kuwaondolea mateso raia wa nchi hiyo.

Hapo juzi Jumanne, Umoja wa Mataifa ulitoa wito wa dola milioni 674 kwa ajili ya miradi ya kiutu nchini Haiti ambako asilimia 45 ya idadi jumla ya watu nchini humo, hawana usalama wa chakula.

Umoja wa Mataifa unasema, mwezi Januari pekee, zaidi ya watu 1,100 waliuwawa, kujeruhiwa au kutekwa nyara.

Kwengineko Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ariel Henry amesema yuko tayari kuunda serikali ya muungano na upinzani hadi pale uchaguzi utakapofanyika.