1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan yaanza kuwazika wahanga zaidi ya 50 wa ugaidi

31 Julai 2023

Pakistan imeanza mazishi ya zaidi ya watu 50 waliouwawa kwenye shambulio la kujitoa muhanga lililoulenga mkutano wa hadhara ulioitishwa na kiongozi wa kidini anayeliunga mkono kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Taliban.

https://p.dw.com/p/4UajU
Pakistan | Beerdigung, Verwandte und Trauernde tragen den Sarg eines Opfers
Picha: Mohammad Sajjad/AP/picture alliance

Mashambulizi hayo ya siku ya Jumapili (Julai 30) yaliwajeruhi watu wengine zaidi ya 200. 

Hakukuwa na kundi lililodai kuhusika lakini mamlaka za Pakistan ziliapa kuwasaka wote waliopanga hujuma hiyo.

Kwenye mashambulizi hayo, mtu mwenye mabomu alijiripua katikati ya mkutano wa wafuasi wa chama cha Jamiat Ulema-e-Islam kinachoongozwa na mwanasiasa na kiongozi wa dini mwenye misimamo mikali, Fazlur  Rehman. 

Soma zaidi: Watu 44 wauawa, 200 wajeruhiwa Pakistan

Hata hivyo, mwazuoni huyo hakuhudhuria mkutano huo uliofanyika kwenye soko moja katika wilaya ya Bajur karibu na mpaka wa Afghanistan.  

Polisi ilisema uchunguzi wao wa awali unaashiria genge lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu ndiyo limehusika.