1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni siku ya kuporomoshwa Ukuta wa Berlin

Sudi Mnette
9 Novemba 2019

Vita Baridi, vita vya dunia kati ya tawala za ukidikteta na kidemokrasia, vilihitimishwa Novemba 9, 1989. Hata hivyo mwenendo wa ulitanguliwa na maamuzi ya matukio kadhaa nje ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/3Sjda
Deutschland Berliner Mauer
Picha: Getty Images/AFP/G. Malie

Siku hii ni kumbukumbu ya ulimwengu kwa utengano wa Ujerumani kwa iliyokuwa Ujerumani Mashariki na Magharibi kwa upande mwingine, na kati ya ukomunisti na ubepari. Ukuta wa Berlin, uliojengwa mnamo mwaka1961 na utawala wa kidiktea wa iliyokuwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani (GDR), ambao pia unaojulikana kama Ujerumani Mashariki.

Berlin Gedenkfeier zum Mauerbau
Mvulana akichungulia katika eneo la mabaki ya ukuta wa BerlinPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Schreiber

Hali ilivyokuwa kabla ya Novemba 9,1989

Ukiwa mzunguko wa kilometa 155, ulijengwa kwa ukuta wa zege na waya, raia wa upande wa Berlin Magharibi, waliishi katika kisiwa cha amani, ikiwa katikati ya utawala wa kikomunisti. Na kwa ka miongo kadhaa, idadi kubwa ya raia wa Ujerumani Mashariki wakizuia kuingia Magharibi, ambako walikuwa wakitamani sana.

Yote hayo yalibadilika mara moja Novemba 9, 1989, pale ambapo serikali ya Ujerumani Mashariki ilipotangaza kwa kupitia mkutano wa waandishi wa habari ambao ulionesha moja kwa moja katika televisheni ya umma. Tangazo hilo lilisema "Mara moja kuanzia sasa, raia wote wa Ujerumani Mashariki wako huru kusafiri kwenda Magharibi." Maelfu ya watu walianza kukimbia kwa kasi kuelekea katika maeneo ya mipaka ya kuingilia katika eneo la kituo cha Berlin ambalo lilipaswa kufungulia katika kipindi cha masaa machache baadae.

Marienborn: Miaka 30 baada ya kuporomoshwa Ukuta wa Berlin

Umuhimu wa siku ya kilele

Ujerumani leo hii inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 30, tangu kupromoshwa kwa ukuta. Wageni kutoka mataifa kadhaa watarajiwa kuhudhuria sherehe rasmi zitakazofanyika mjini Berlin. Rais wa Shirikisho  Frank-Walter Steinmeier na Kansela Angela Merkel watashirikia katika maadhimisho ya kitaifa ya mjini Berlin. Lakini baadae jioni Steinmeier ataungana na wasanii wengi pamoja na mashuhuda wengine katika tamasha kubwa na vilevile atazungumza na wahudhuruaji. Mbali na hayo maandamano yamepangwa kufanyika katika maeneo mbalimbali ya kihistoria ya mapinduzi hayo ya amani ya mwaka 1989.