1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Mshauri wa usalama wa Taifa wa Marekani azuru Israel

19 Mei 2024

Ndege za kivita na vifaru vya jeshi la Israel vimeyashambulia maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza leo Jumapili.

https://p.dw.com/p/4g3KU
Mzozo wa Gaza
Mzozo wa Gaza Picha: picture alliance/dpa

Yamefanyika katika wakati afisa wa ngazi ya juu wa utawala wa Marekani anafanya ziara nchini Israel kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Mashambulizi makali yameripotiwa kwenye eneo la Jabalia ambako kuna kambi kubwa ya wakimbizi wa Kipalestina.

Mapema hii leo, Jake Sullivan, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani alikutana na Netanyahu akilenga kufikisha ujumbe wa Washington wa kuitaka Israel kutotumia nguvu kubwa kwenye oparesheni yake ya mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah.

Vikosi vya Israel vimekuwa vikisonga mbele kwenye mji huo ambao inasema ndiyo ngome ya mwisho ya wanamgambo wa Hamas.

Jumuiya ya kimataifa imeionya mara kadhaa Israel kutoushambulia kwa sababu mji huo unawahifadhi mamia kwa maelfu ya Wapalestina waliokimbia vita maeneo mengine ya Gaza.