1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkurugenzi wa moja ya gereza kuu nchini Colombia auawa

17 Mei 2024

Mkurugenzi wa mojawapo ya gereza kubwa nchini Colombia ameuawa jana mjini Bogota baada ya kupokea vitisho kutoka kwa wafungwa.

https://p.dw.com/p/4fxtq
Colombia-Bogota
Mojawapo ya kitongoji cha mji wa BogotaPicha: ALEJANDRO MARTINEZ/AFP

Mkurugenzi wa mojawapo ya gereza kubwa nchini Colombia ameuawa jana mjini Bogota baada ya kupokea vitisho kutoka kwa wafungwa. Hayo yameelezwa na Rais wa nchi hiyo Gustavo Petro aliyetangaza kuwa Kanali Mstaafu Elmer Fernández ameuawa alipokuwa kwenye gari lake.

Soma: Jeshi la Colombia lamkomboa Betancourt

Fernández ambaye alichukua wadhifa huo Aprili 4, alikuwa akitekeleza maagizo ya kinidhamu na kufanya upekuzi katika gereza hilo linalofamika kama  " La Modelo". Rais Petro ametangaza kuundwa kwa Baraza la Usalama litakalojadili hatua za ziada zinazotakiwa kuchukuliwa kwa magereza yote nchini humo.

Colombia, mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa dawa za kulevya aina ya kokeini na huwa haikabiliwi na kiwango cha vurugu kwenye magereza kama zinazoshuhudiwa katika magereza ya Ecuador, ambako vitendo vya mauaji na ufyatuaji risasi vimekuwa vikiripotiwa katika miezi ya hivi karibuni.