1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yauwa 35 Gaza

Sudi Mnette
1 Januari 2024

Mashambulizi ya jeshi la Israel yamesababisha vifo vya takriban watu 35 katika mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4akfY
Nahostkonflikt Gaza
Picha: Mohammed Dahman/AP Photo/picture alliance

Taarifa hiyo ya Jana Jumapili ni kwa mujibu wa maafisa wa hospitali.Vifo hivyo vinatokea katika eneo hilo lililozingirwa ikiwa ni takriban siku moja tu, baada ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kusema vita vya vitaendelea kwa miezi mingine zaidi, akikaidi miito ya kimataifa ya kusitisha vita.Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vimekuwa vikiendelea na operesheni zake za kijeshi za mji wa pili kwa ukubwa wa Gaza, wa Khan Younis, ambapo wakazi wanatoa taarifa ya kutokea mashambulizi katika eneo la katikati. Israel inasema inataka kuvuruga utawala wa Gaza na uwezo wa kijeshi wa  Hamas, ambao mnamo Oktoba 7 walilishambulia eneo la kusini mwa Israel, ambayo nayo ikaanzisha mashambulizi ya kisasi dhidi ya kundi hilo.