1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marienborn: Kumbukumbu ya historia ya Ujerumani iliyogawika

Admin.WagnerD8 Novemba 2019

Kwa takribani miaka 40, Ujerumani iligawanywa kwa ukuta ambao lengo kwa mtazamo wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki lilikuwa kuwazuia raia wake wasiweze kujihusisha au kuzipata fikra za kifashisti.

https://p.dw.com/p/3SfXd
Berlin Grenzübergang Helmstedt/Marienborn
Picha: DW/N. Amadou

Katika kipindi hicho zaidi ya watu 100,000 walifanya jaribio la kuutoroka upande huo na 5,000 walifanikiwa kwa kuuparamia ukuta uliozigawa pande hizo. Katika kuelekea kumbukumbu ya miaka 30 toka ulipoangushwa ukuta wa Berlin  Sudi mnette ni miongoni mwa waandishi wanne waliopata fursa ya kwenda kujionea hali ilivyo upande wa Mashariki na kutuandalia ripoti ifuatayo.

Katika harakatu za kuruka ukuta, idadi kubwa ya watu iliuwawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa mipakani, baadhi ya ripoti zinasema kiasi ya watu 1,000 waliuwawa katika harakati za kutaka kuvuka kizuizi.  Marienborn ni kituo kikubwa kabisa cha ukaguzi. Zilikuwa nyakati za alasiri DW ilipowasili katika eneo la ukaguzi la Marieborn. Eneo hilo lilionekana kuwa na viwanja vya wazi vikumwa ambavyo kama utavijumuisha kwa pamoja inawezekana kupindukia viwanja vya mpira wa miguu 30.

Berlin Grenzübergang Helmstedt/Marienborn
Kibanda cha wakaguzi wa ushuru wa forodhaPicha: DW/N. Amadou

Hali ya sasa ya Marienborn miaka 30 baada ya kuporomoshwa ukuta

Hadi katika kipindi hiki ambacho Wajerumani wanakumbuka miaka 30 ya kuvunjwa kwa ukuta huo, eneo hilo linaonekana kuwa na vibanda ambavyo, vilitumika mahusisi kwa udhibiti wa safari kutoka Mashariki na kuingia Magharibi, kadhalika upande huo pia na kurejea Mashariki. Hapo na mahala na kukagua pasipoti, ushuru wa forodha na mengine kama hayo. Rekodi zinaonesha eneo hilo lilijiengwa miaka ya 1975, kwa dhamira ya kuweza kuhudumia magari mengi katika zama hizo za utengano.

Eneo hilo la ukaguzi, halikutumika tu kwa ajili ya iliyokuwa Ujerumani Mashariki na Magharibi, bali pia wasafiri wengine kutoka Poland. Angelika Maedicke ni mwanahistoria, mzaliwa wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki ikifahamika kama GDR na anafanya kazi katika kituo hicho cha ukaguzi kwa zaidi ya miaka 16. Zaidi Angelika Maedicke alisema "Kulikuwa na watu wachache sana kutoka Ujerumani Mashariki ambao walikuwa wakipita katika kituo hiki cha ukaguzi. Idadi kubwa ya walipita hapa kwa magari walikuwa wafanyabiashara na malori na wanadiplomasia. Fursa ilitolewa kwa watu wa Mashariki, pale Kansela Willy Brand aliposisitiza kulegezewa masharti kwa wale walikuwa na changamoto za kimaumbile na kutaka kuingia Magharibi."

Berlin Grenzübergang Helmstedt/Marienborn
Hati za kuvuka eneo la mpakaPicha: DW/N. Amadou

Adhabu kali kwa mtu anavuka kuingia Ujerumani Magharibi bila ya ridhaa

Eneo hilo la mpaka lilikuwa ni eneo muhimu la mamlaka ya Ujerumani Mashariki, kudhibiti usalama wake wa mipakani. Lakini jitihada hiyo ya udhibiti haikuishia katika eneo la mipaka tu, yeyote anahusisha na njama za kutaka kutoroka upande huo anaweka chini ya uangalizi mkali kwa miaka kadhaa, kufanyiwa upekuzi nyumbani na baadhi yao waliweza hata kutumika kifungo baada ya kukutwa na hatia. Katika kipindi hicho kulikuwa hakuna hali ya kuaminiani kwa upande wa Ujerumani Mashairiki-GDR. Lakini yako wa karibu kabisa anaweza kuwa mpelelezi. Friedhart Knolle ni  raia ambae kwa wakati huo alikuwa akitokea upande wa Ujerumani Magharibi ambae amekuwa akufuatiliwa na mamlaka ya iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa miaka mingi sana, kwa vile tu alikuwa na marafiki zake upande huo. Zaidi alisema "Miaka kadhaa baada ya kuungana upya mmoja kati ya watu hao alinifuata na kusema Friedhart, twende upande mwingine wa mtaa ambako hakuna mtu yoyeto. Nipaswa kukueleza kitufulani na alizungumza kwa maneno mazuri kwa kiasi cha dakika tano, alisema kimsingi kuna rekodi kubwa kukuhusu kwa serikali ya Ujerumani Mashariki, na nakueleza utaweza kuona pia jina langu katika rekodi hizi. Alikuwa mtu mwenye maarifa. hakuwa mtu mbaya."

Lakini kimsingi ilikuwa wasiwasi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki dhidi ya vijana wasomi kutoka Magharibi, na shabaha ileile ya kudhibiti fikra za kifashisti zisitamalaki katika eneo la Mashariki, ambalo kwa wakati huo lilifuata mrengo wa kisovieti kupinganga na Umagharibi. Kwa hivi sasa kituo cha Marienborn kimesalia kuwa kumbukumbu muhumi wa Ujerumani iliyogawika.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri:Yusuf Saumu