1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu

12 Septemba 2023

Marekani inakaribia kuidhinisha msaada wa makombora ya masafa marefu kwa Ukraine, na hivyo kuipatia Kyiv uwezo wa kupambana vilivyo na vikosi vya Moscow hasa katika maeneo yaliyonyakuliwa kinyume cha sheria na Urusi.

https://p.dw.com/p/4WDhS
USA US-Präsident Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

 Makombora hayo ni ya kisasa na yenye uwezo mkubwa.

Kwa muda wa miezi kadhaa, utawala wa Rais Biden umekuwa ukitatizika kuchukua uamuzi wa kutumwa kwa makombora hayo (ATACMS), kwa hofu kwamba usafirishaji wake ungelichukuliwa kama hatua ya uchokozi dhidi ya Urusi.

Lakini Ukraine imekuwa ikihimiza kupewa makombora hayo.

Soma pia:Marekani yaipa Ukraine msaada wa dola bilioni moja

Hadi sasa hakuna uamuzi wa mwisho uliofikiwa na haikuwa wazi ikiwa silaha hizo zingejumuishwa katika shehena ijayo ya msaada wa silaha kwa Ukraine.

Aina hiyo ya makombora imepigwa marufuku na zaidi ya nchi 100 lakini Urusi, Ukraine na Marekani hazikusaini Mkataba huo.