1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron: Ulaya haipaswi kujitenga na China

5 Aprili 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Ulaya lazima ijiepushe kupunguza mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na China, wakati akianza ziara ya kiserikali mjini Beijing leo.

https://p.dw.com/p/4PjwH
China | Emmanuel Macron akiwa mjini Beijing
Rais Emmanuel Macron akizungumza na raia wa Ufaransa waishio China wakati wa siku yake ya kwanza ya ziara nchini humo.Picha: Thibault Camus/AP/picture alliance

Macron ambaye yuko katika ziara ya siku tatu nchini China pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wanalenga kufuta dhana yoyote kuwa kuna mvutano usioepukika kati ya Beijing na Nchi za Magharibi.

Macron amesema kuendeleza mazungumzo na China ni muhimu ikizingatiwa mahusiano yake ya karibu na Urusi, ambayo inaendesha vita nchini Ukraine.

Kwingineko, Rais wa Ukraine alizuru leo nchini Poland na kuishukuru nchi hiyo kwa kile alichokiita msaada wa kihistoria, akisema inapaswa kuwa mshirika muhimu katika juhudi pana za ujenzi unaohitajika wakati uvamizi wa Urusi utakapomalizika.

Rais wa Poland Andrej Duda alisema Poland itapeleka Ukraine ndege za kivita 14 aina ya MiG-29.