1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipi kilivisibu vilabu vya Ujerumani Mashariki?

Iddi Ssessanga
2 Oktoba 2020

Baada ya kukamlika kwa muungano wa Ujerumani miaka 30 iliyopita, klabu za juu za Ujerumani Mashariki zilijumlishwa kwenye piramidi ya Bundesliga. Lakini zilipambana kushindan na baadhi vilabu vikubwa vimeshuka madaraja.

https://p.dw.com/p/3jMp0
Fußball l Achter DDR-Meistertitel für den BFC Dynamo - 1986
Picha: picture-alliance/A. Altwein

Miaka 30 tokea muungano wa kihistoria wa Ujerumani, mijadala bado inaendelea kuhusu namna suala hilo limekuwa na unafanisi. Kuanzia siasa na umri hadi ajira na uzalishaji wa kiuchumi, tofuati kubwa zinasalia kati ya majimbo 11 "ya zamani" ya iliyokuwa Ujerumani Magharibi, na majimbo matano "mapya" ya Ujerumani ya kikomunisti ya Mashariki. Na soka pia haiko tofauti.

Hususani katika miaka ya 1970 na 1980, klabu ya Jamhuri ya zamani ya Kidemokrasia ya Ujerumani (GDR) zilikuwa zinawakilishwa katika hatua za mwisho za mashindano ya Ulaya.

Magdenburg ilishinda kombe la mshindi la Ulaya mnamo mwaka 1974 huku Carl Zeiss Jena na Lokomotive Leipzig zote zikifika katika ngazi ya fainali ya mashindano hayo.. Dyanamo Dresden ilicheza rekodi ya mechi 98 za Ujerumani Mashariki katika michezo ya Ulaya.

Kufuatia kuungana upya kwa Ujerumani, klabu za ligi kuu ya Ujerumani Mashariki - Oberliga zilijumuishwa kwenye piramidi ya Ujerumani Magharibi. Mbili za juu ziliongezwa kwenye Bundesliga, ya tatu hadi sita zikajiunga na ligi ya daraja la pili, wakati ya saba hadi 12 zilishiriki mechi za kufuzu kwa ajili ya daraja la pili.

Kufikia 2020 hata hivyo, hakujawahi kuwepo zaidi ya klabu mbili za Ujerumani mashariki katika msimu wowote wa Bundesliga. Msimu huu, ni Union Berlin na RB Leipzig zilizo na makao yake katika iliyokuwa GDR, ingawa Leipzig iliundwa kiutata tu 2009. Kuna timu moja tu zaidi ya mashariki kwenye ligi ya daraja la pili: Erzgebirge Aue, ikijulikana wakati wa GDR lama Wismut Aue.

Kipi kilizisibu nyingine?

Hansa Rostock (daraja la tatu)

Mabingwa wa mwisho kabisaa wa Ujerumani Mashariki, Hansa Rostock, walifuzu moja kwa moja kuingia Bundesliga baada ya ushindi wa kushangaza wa Oberliga msimu wa 1990-91.

Fußball Hansa Rostock feiert Bundesliga-Aufstieg
Hansa Rostock wakisherehekea ushindi wa kombe la mwisho la Oberliga mjini Rostock Mei 28, 1991.Picha: picture alliance/dpa/B. Wüstneck

Ingawa walishushwa daraja katika msimu wao wa kwanza, klabu hiyo kutoka pwani ya Baltic ilirejea na walikuwa katikati mwa msimamo wa Bundesliga kutoka 1995-2005. Wakiwa na juml ya  misimu 12 ya Bundesliga, hakuna klabu ya mashariki ilkaa muda zaidi katika ligi iliyoungana na Ujerumani kuliko Hansa.

Tangu 2013 hata hivyo, Rosctock wamejikuta wakikwama katika ligi ya daraja la tatu, ambamo wamemaliza katika nafasi ya sita katika misimu mitatu iliyopita. Bado wanavutia makundi ya mashabiki zaidi ya 12,000 na wanajivunia moja ya mandhari ya mashabiki wenye fujo zaidi nchini Ujerumani.

Dynamo Dresden (daraja la tatu)

Mabingwa mara nane wa Ujerumani Mashariki na washindi mara saba wa kombe wa washindi Dynamo Dresden walimaliza wa pili katika msimu wa mwisho wa Oberliga, na pia kufuzu moja kwa moja kushiriki ligi ya Bundesliga mwaka 1991, ambako walibakia kwa misimu minne.

Fußball Berlin Fans von Dynamo Dresden zünden bengalisches Feuer
Dynamo Dresden, daraja la tatu. Picha: picture-alliance/dpa/A. Gora

 

Mwaka 1995 hata hivyo, wakizama katika madeni, walishushwa moja kwa moja hadi daraja la tatu. Kufikia mwisho wa Milenia, marekebisho ya piramidi ya ligi yaliwashuhdia waliporomoka hadi ligi ya daraja la nne.

Tangu wakati huo, wamepanda taratibu, shukuran kwa msaada w akifedha - msimu uliyopita, zaidi ya mashabiki 30,000 wa Dynamo walisafiri kwenda Hertha Berlin kucheza ugenini katika kombe la Ujerumani -- na uwanja mpya na wa kisasa.

Katika kipindi cha muongo uliyopita walionekana timu iliyotulia katika daraja la pili, na hata wakajaribu kupanda daraja hadi Bundesliga mwaka 2017. Lakini msimu uliyipita, walishushwa tena hadi daraja la tatu.

Magdeburg (daraja la tatu)

Klabu pekee ya Ujerumani Mshariki kushinda kombe kubwa la Ulaya, ikiipiga AC Milan na kushinda Kombe la Washindi katika fainali ya 1974, Magdenburg inaweza kujigamba kuwa timu iliyopta ushindi mkubwa zaidi katika GDR.

Mshambuliaji wa klabu hiyo Jürgen Sparwasser oia alifunga goli la ushindi katika ushindi maarufu wa kombe la dunia wa Ujerumani Mashariki dhidi ya Ujerumani Magharibi mjini Hamburg miezi michache baadae.

Fußball DFB Pokal Christian Beck Magdeburg 11 vorne Jubel nach Spielende Freude über den Sieg Erfolg success b
Wachezaji wa klabu ya Magdenburg wakisherehekea ushindi dhidi ya FC Augsburg, 13.08.2017.Picha: Imago/foto2press

Hata hivyo kufikia wakati wa muungano, klabu hiyo kutoka Saxony-Anhalt ilimaliza katika nafasi ya 10 na iliendelea kucheza katika ligi za daraja la tatu na nne kwa sehemu kubwa ya miongo mitatu, ikipambana pia na ufilisi.

Hatimaye mwaka 2015, walirejea kwenye ligi yatatu inayochezwa kitaifa, wakipata ushindi wa kihitoria uliyopelekea kupandishwa daraja kabla ya kurejea moja kwa moja tena chini.

Kama ilivyo kwa mahasimu wao Hansa na Dynamo, mashabiki wa Magdenburg pai wanasifika kwa fujo.

BFC Dynamo (daraja la nne)

Katika kandanda la Ujerumani Mashariki, kitangulizi cha "Dynamo" kilimaanisha klabu iliyokuwa inasaidiwa na polisi ya siri - Stasi. Zilikuwa zinapatiwa wachezaji bora zaidi nchini na zilikuwa zinachukiwa na mashambiki wapinzani kutoka kudhaniwa kupendelewa na waamuzi - na zaidi hasa klabu ya BFC Dynamo.

Klabu hiyo ya Berlin Mashariki fahari ya mkuu wa Stasi Erich Mielke na ilishinda rekodi ya mataji kumi ya Oberliga mfululizo kati ya 1979 na 1988. Kufikia msimu wa mwisho wa Oberliga hata hivyo, ikicheza kwa jina la FC Berlin na bila uungwaji mkono wa Stasi, walikosa kuingia katika Bundesliga.

Fussball l Das Sportforum Berlin in Hohenschönhausen
BFC Dynamo, daraja na nne.Picha: picture-alliance/K. Kleist-Heinrich

Tangu wakati huo, BFC imekuwa ikilaaniwa kama klabu ya Stasi kutokana na historia yake na klabu ya Manazi kutokana na wahuni wake - lakini pia ikipendwa kama klabu ya jamii na mashabiki wanaoendelea kuwa watiifu.

Carl Zeiss Jena (daraja la nne)

Ikiundwa mwanzoni kabisaa mwaka 1903 kama timu ya wafanyakazi wa kampuni ya miwani ya Cark Zeiss, Jena iliendelea na kuwa moja ya timu maarufu zaidi katika GDR. Ilishinda Oberliga mara tatu, kombe la Ujerumani Mashariki mara nne na ilitinga fainali ya kombe la Ulaya mwaka 1981, na kushindwa na Dinamo Tibilisi ya Georgia.

Licha ya kufuzi kwa daraja la pili mwaka 1991, Jena imekaa misimu nane tu kwa ngazi hiyo tangu wakati huo, ikicheza kati ya ligi za daraja la tatu na nne. Miaka mitatu mfululizo katika ligi ya tatu ilikomeshwa msimu uliyopita wakati Jena ilipomaliza ya mwisho kabisaa ikiw aimeshinda michezo mitano tu na kupigwa magoli 85.

FC Carl Zeiss Jena | Trainer Hans Meyer
Kocha wa FC Carl Zeiss Jena, Hans Meyer.Picha: Imago/Camera 4

Mpira unaweza kuwa ulikuwa mbaya uwanjani, lakini mitazamo katika uwanja wa michezo wa Ernst-Abbe mjini Jena ndiyo miongoni mwa ya kustajaabisha zaidi nchini Ujerumani. Paviliano ya kusini ni nyumbani kwa wakereketwa wa klabu hiyo, wa Horda Azzuro, ambao ni moja ya makundi ya mashabiki yenye kuendelea katika soka la Ujerumani Mashariki.

Lokomotive Leipzig (daraja la nne)

Karibu sana, lakini mbali sana - yumkini hiyo ndiy njia bora ya kuilezea Lokomotive Leipzig, ambayo mtangulizi wake VfB Leipzig walikuwa mabingwa wa kwanza kabisaa wa Ujerumani mnamo 1903.

Wakati wa miaka ya GDR, Lok Leipzig ilishinda vikombe vinne vya Ujerumani Mashariki lakini walikuwa timu iliyoshindwa kwenye fainali tatu. Walimaliza pia wa pili mara tatu katika Oberliga na walipoteza kwa Ajax katika fainali ya kombe la washindi la Ulaya mnamo 1987.

Fußball Lok Leipzig Fans
Mashabiki wa Lok Leipzig.Picha: picture-alliance/dpa/P. Endig

Licha ya kampeni moja ya Bundesliga mwaka 1993 -1994 (wakiwa wamerudi chini ya jina la VfB), klabu hiyo ilishushwa hadi daraja la nne na ilisambaratika mwaka 2004, kabla ya kuundwa upya na mashabiki na kupanda hadi daraja na nne.

Msimu uliyopita, baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la virusi vya corona, Lok walikuwa wametawazwa mabingwa kwa alama za mchezo lakini walipoteza mechi ya kuamuka dhidi ya SC Verl kwa magoli ya ugenini. Walikuwa karibu, lakini mbali sana.

Energie Cottbus (daraja la nne)

Kabl ya kupandishwa kwa Union Berlin mwaka 2019, klabu ya mwisho kutoka GDR ya zamani kucheza Bundesliga ilikuwa Energie Cottbus, iliyoshushwa mwaka 2009.

Timu hiyo kutoka Brandenburg, karibu na mpaka wa Poland, haikuwa na makali katika Ujerumani ya Mashariki. Waliweza tu kucheza kwa miaka sita katika Oberliga, na hawakufikia ngazi za kimataifa za vilabu vingine vilivyotajwa hapa. Hawakufuzu hata kwa daraja la pili baada ya muungano lakini waliweza kupanda daraja hadi Bundeliga kufikia mwaka 2000.

Deutschland Fußball Regionalliga | FC Energie Cottbus vs. 1. FC Lok Leipzig
FC Energie Cottbus ikicheza dhidi ya FC Lok Leipzig, Februari 08, 2020.Picha: picture-alliance/Fotostand/Weiland

Miaka 14 katika ligu mbili za juu ilifuatia kabla ya kushuka hadi ligi ya daraja la tatu na kisha daraja la nne, ambako wanasalia hadi hii leo.

Energie wamepamba zaidi vichwa vya habari nje ya uwanja katika miaka ya karibuni kutokana na uwepo na wafuasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia miongoni mwa mashabiki wake - lakini mashabiki wengine wa Cottbus wamedhamiria kuboresha taswira ya klabu hiyo.