1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa makumbusho ya Yad Vashem kuizuru Ujerumani

18 Januari 2023

Mkuu wa makumbusho ya mauaji ya halaiki dhidi ya Wayahudi ya Yad Vashem nchini Israel, Dani Dayan anatarajiwa kufanya ziara nchini Ujerumani, ya kwanza maishani mwake.

https://p.dw.com/p/4MO6n
DW Interview mit Dani Dayan Vorstandsvorsitzender der Gedenkstätte Yad Vashem
Picha: DW

Mkuu wa makumbusho ya mauaji ya halaiki dhidi ya Wayahudya Yad Vashem nchini Israel, Dani Dayan anatarajiwa kufanya ziara nchini Ujerumani, ya kwanza maishani mwake.

Katika mahojiano maalumu na DW Dayan amesikitika kwamba chuki dhidi ya Wayahudi imeenea tena duniani. Amesema hiyo ndio sababu huwa anawahimiza viongozi wa dunia wanaoyatembelea makumbusho ya Yad Vashem kuchukua hatua za haraka mara tu waonapo dalili za chuki dhidi ya Wayahudi, kwa kuwa wakichelewa chuki hiyo itafika katika kiwango kisichoweza kudhibitiwa.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa makumbusho ya Holocaust amesema hali ya leo ni tofauti na ya miaka 80 iliyopita, kwa sababu hivi sasa watu wanatambua hatari inayoweza kutokea, akasisitiza lakini jukumu la kila mmoja katika kupinga chuki dhidi ya Wayahudi, ubaguzi wa rangi na kutovumiliana.