1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Hamas kuhudhuria mazungumzo ya kusitisha vita

Sylvia Mwehozi
1 Februari 2024

Kiongozi wa kundi la Hamas anatarajiwa kuwasili mjini Cairo nchini Misri leo kwa mazungumzo kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4bvx8
Diplomasia na Siasa | Mkuu wa masuala ya Kisiasa Hamas, Ismail Haniyeh
Mkuu wa masuala ya Kisiasa Hamas Ismail Haniyeh akizungumza na vyombo vya habari.Picha: Cem Tekkesinoglu/AA/picture alliance

Chanzo kimoja kimelieleza shirika la habari la AFP kwamba Hamas ilikuwa inapitia pendekezo la kusitisha vita kwa wiki sita katika vita vyake na Israel.

Hatua hiyo inakuja baada ya wapatanishi kukusanyika mjini Paris huku juhudi za jumuiya ya kimataifa zikielekezwa katika kutafuta usitishaji mpya wa mapigano katika mzozo huo.

Soma pia:Netanyahu: Sitaridhia makubaliano ya kusitisha mapigano

Huko Gaza kwenyewe, Israel imeendeleza mashambulizi huku mwelekeo ukiwa ni katika mji mkuu wa kusini wa Khan Younis, ambako Israel inadai kwamba viongozi wa Hamas wamejificha.

Usiku kucha, mashahidi wameelezea mashambulizi kadhaa ya anga ya Israel huku wafanyakazi wa misaada na afya nao wakiripoti mapigano mazito kwa siku kadhaa.