1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Biashara

Kenya, EU zasaini makubaliano "ya kihistoria" ya biashara

18 Desemba 2023

Kenya na Umoja wa Ulaya zimetia saini hii leo makubaliano ya kibiashara yaliyojadiliwa kwa muda mrefu ili kuongeza mtiririko wa bidhaa kati ya masoko hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4aIQN
Kenya | Urusula von der Leyen na William Ruto
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akiwa na rais wa Kenya William Ruto.Picha: State House of Kenya/Andalou/picture alliance

Hayo yamefahamishwa na Rais William Ruto katika wakati ambapo Brussels ikilenga kukuza mahusiano ya kiuchumi na bara la Afrika.

Ruto amesema huo ni mwanzo wa ushirikiano wa kihistoria utakaopelekea pia mabadiliko ya kihistoria. Rais huyo wa Kenya aliyasema hayo katika hafla iliyohudhuriwa na rais wa Hamlashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Soma pia: Kenya inatafuta utulivu wa kiuchumi baada ya miaka 60 ya uhuru

Von der Leyen amesema ushirikiano huo ni wa manufaa kwa pande zote mbili na kutoa wito kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki kujiunga na makubaliano hayo ya ushirikiano wa kiuchumi.