1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Scholz kulihutubia Bunge kuhusiana na matatizo ya bajeti

24 Novemba 2023

Ofisi ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz imetangaza kuwa kiongozi huyo anapanga kulihutubia Bunge Ijumaa wiki ijayo kuhusiana na mkwamo wa bajeti unaoikabili serikali yake.

https://p.dw.com/p/4ZQQV
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Waziri wa Uchumi Robert Habeck na Waziri wa Fedha Christian Lindner
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Waziri wa Uchumi Robert Habeck na Waziri wa Fedha Christian LindnerPicha: Ben Kriemann/Pic One/picture alliance

Hatua hii ni baada ya Mahakama ya Shirikisho kutoa uamuzi unaoizuia kuchukua mkopo wa mabilioni ya euro.

Serikali ya mseto ya Kansel Scholz inakabiliwa na msukosuko wa kibajeti kutokana uamuzi wa mahakama wa Novemba 15, uliosema mipango ya kuchukua  mkopo wa dola bilioni 65,4 kufadhili miradi ya kimkakati ni kinyume na katiba.

Soma pia: Rungu la Mahakama latikisa sehemu ya bajeti ya Ujerumani

Mahakama hiyo ilisema serikali ya Scholz imevunja masharti ya katiba kwa kukiuka ibara inayoweka ukomo wa deni la taifa kupitia azma yake ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili yakukabiliana na janga la UVIKO-19kwenda kwenye mfuko wa kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Uamuzi huo umeibua maswali kuhusu ni jinsi gani serikali ya Scholz itafadhili miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, ujenzi na ukarabati wa miundombinu pamoja na mpango wa ruzuku ya kukabiliana gharama kubwa za nishati ya gesi na umeme.