1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema mateka wake mwingine amefariki dunia Gaza

Lilian Mtono
3 Mei 2024

Serikali ya Israel imesema mateka mwingine wa taifa hilo anayeshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza amefariki.

https://p.dw.com/p/4fTD8
 Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Maya Alleruzzo/AP/dpa/picture alliance

Katika tangazo lake la usiku wa jana kupitia mtandao wa kijamii wa X, Israel imesema mwili wa mateka huyo bado uko Gaza. Haikuelezwa muda wala chanzo cha kifo hicho na chanzo hasa cha taarifa hizo pia hakijajulikana.

Itachukuwa miaka 16, dola bilioni 40 kuijenga tena Gaza - UM

Katika hatua nyingine, Waziri wa Biashara wa Uturuki Omer Bolat amesema hawatarejesha uhusiano wa kibiashara na Israel hadi kutakapofikiwa makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuondoa vikwazo vya ufikishwaji wa misaada ya kiutu kwenye eneo hilo. 

Uturuki jana Alhamisi ilitangaza kusitisha biashara zote na Israel ikiangazia kuzorota kwa hali ya kiutu huko Gaza.