1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hamas yazingatia pendekezo la mapatano na Israel

Iddi Ssessanga
3 Februari 2024

Maafisa wa Hamas wanasema kundi hilo lilikuwa linachunguza pendekezo la usitishaji vita, ambalo linahusisha usimamishaji mapigano uliorefushwa Gaza, na ubadilishanaji wa mateka na wafungwa.

https://p.dw.com/p/4bzm7
Vita vya Israel-Hamas
Hamas imesema itajivu pendekezo la kusitisha mapigano na IsraelPicha: IDF/Handout/REUTERS

Maafisa wa Hamas wamesema jana kuwa kundi hilo lilikuwa linachunguza pendekezo la usitishaji vita, ambalo linahusisha usimamishaji mapigano uliorefushwa Gaza, na ubadilishanaji wa mateka wa Israel kwa wafungwa wa Kipalestina.

Hata hivyo Hamas ilionekana kupinga baadhi ya vipengele muhimu katika pendekezo hilo. Kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh alisema majadiliano laazima yakomeshe kabisaa operesheni za kijeshi za Israel na kuleta uondoaji wa vikosi vyake Gaza. Israel inapinga masharti hayo.

Soma pia: UNCEF yasema watoto 17,000 Gaza hawana ndugu wa karibu

Afisa wa Hamas mjini Beirut Osama Hamdan, alisema kundi hilo litataka kuachiwa kwa maelfu ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwa vitendo vinavyohusiana na mzozo na Israel.

Haijabainika wazi lini na iwapo Hamas itatoa jibu la wazi kuhusu pendekezo hilo au kutoa pendekezo mbadala. Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumani na serikali nyingine kadhaa zinaichukulia Hamas kuwa shirika la kigaidi.