1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COVID-19 yauwa zaidi ya Wamarekani 200,000

Sudi Mnette
23 Septemba 2020

Idadi ya waliokufa kutokana na janga la virusi vya corona nchini Marekani imepindukia watu 200,000, ikiwa ni kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins,

https://p.dw.com/p/3irdm
USA | Coronavirus | Kansas | Mann mit Mundnasenschutzmaske
Picha: picture-alliance/AP Photo/C. Riedel

Hatua hiyo mbaya imefikiwa baada ya takribani miezi saba tangu Marekani itangaze kifo chake cha kwanza kilichotokana na janga la virusi vya corona, mwishoni mwa Februari. Markani ndilo taaifa lenye idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi vya corona duniani.

Kwa sasa Marekani ina asilimia 20 ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo. Vilevile taifa hilo linaongoza kwa kuyaacha umbali mrefu mataifa mengine likiwa na visa vya maambukizi milioni 6.8, na kufuatiwa na India yenye maambukizi milioni 5,56 na vifo 88,935. Na Brazil maambukizi milioni 4.57 na vifo 138,159.

Wamarekani hawafurahishi na serikali yao inavyoshughulikia virusi vya corona.


Idadi kubwa ya raia wa Marekani hawafurahishi na serikali yao, kwa namna invayoshghulikia janga la virusi vya corona, ingawa Rais Donald Trump ambae anawania muhula wake wa pili madarakani katika uchaguzi wa Novemba, 3 amekuwa akijinasibu kuchukua hatua stahiki.

USA I UN-Generalversammlung I Donald Trump
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: UNTV/AP/picture-alliance

Hata hivyo Trump kama kawaida yake alitaja China na kutupa lawama kidoko kwa kusema kama ingaliweza kulidhibiti janga hilo katika mipaka yake yasingetokea yanayotokea sasa. Kwengineko nchini Mexico, wizara ya afya ya nchi hiyo inasema idadi ya maambukizi imeongezeka na kufikia watu 705,263 huku vifo vikiwa 74,348. Serikali inasema visa vipya ni  vyacorona4,683 na vifo 651. Inaonekana idadi hiyo inaweza kuwa ndogo zaidi kuliko hali halisi kutokana na uwepo wa idadi ndogo ya watu wanaopimwa.

Viongozi kwenye Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa wahimiza chanjo ya COVID-19.

Janga la virusi vya corona limeweza kupata nafasi kubwa katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa ambayo imeanza kwa njia ya vidio hapo Jana Jumanne. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Anthonio Gutteres amonya kwamba dunia inakabiliwa na janga kubwa ambalo litaathiri uchumi wa dunia, hatari kwa haki za binaadamu na kuchochea vita baridi kati ya China na Marekani. Rais wa Argentina Albertor Fernandez ameutaka ulimwengu kusugua kichwa katika kutafuta chanjo ya virusi hivyo huku Emmanuel Macron wa Ufaransa akisema corona lazima iuamshe ulimwengu katika kufanya kazi pamoja.

Vyanzo: APE/APTN/DPAE