1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Ujerumani AfD kujiimarisha siasa za Ulaya

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Wajumbe wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia wa chama Mbadala kwa Ujerumani AfD, jana walikusanyika katika mji wa Mashariki mwa Ujerumani wa Magdeburg kuanza mkutano wao wa kila mwaka utakaodumu hadi Jumapili.

https://p.dw.com/p/4UXD8
Alice Weidel wa AfD-mjini Magdeburg
Kiongozi mwenza wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani (AfD) Alice Weidel katika mkutano wa MagdeburgPicha: AFP

Wajumbe wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia wa chama Mbadala kwa Ujerumani AfD, jana walikusanyika katika mji wa Mashariki mwa Ujerumani wa Magdeburg kuanza mkutano wao wa kila mwaka utakaodumu hadi Jumapili.

Katika siku ya kwanza ya mkutano, uongozi wa chama hicho umeapa kuongeza ushiriki wake katika ngazi ya Ulaya. Wajumbe walipiga kura kuidhinisha nia ya uongozi ya kujiunga na chama chenye itikadi sawa katika bunge la Umoja wa Ulaya cha European Identity and Democracy ID. Chama hicho cha ID kiliundwa mwaka 2019 kikijumuisha vyama vyenye siasa kali kutoka nchi 9 za Umoja wa Ulaya.

Soma pia: Chama cha siasa kali cha AfD chashika nafasi ya pili Ujerumani

Kwa kujiunga rasmi na chama hicho, AfD inatarajia kupokea ruzuku zaidi kutoka Brussels. AfD imesema kuwa chama cha ID ni jukwaa zuri la kuendelea kupanua mtandao wa vyama dada vya AfD ndani ya Ulaya.