1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso Mali na Niger zakamilisha mpango wa ushirikiano

Amina Mjahid
18 Mei 2024

Serikali zinazoongozwa kijeshi za Burkina Faso, Mali na Niger zimesema zimekamilisha mipango ya kuunda muungano wao wa pamoja baada ya kuligeuka koloni lao la zamani Ufaransa na kujisogeza karibu zaidi na Urusi.

https://p.dw.com/p/4g1x6
 Assimi Goïta, Abdourahamane Tiani, Ibrahim Traoré
Viongozi wa kijeshi wa Mali Assimi Goïta, Niger Abdourahamane Tiani na mwenzao wa Burkina Faso Ibrahim Traoré Picha: Francis Kokoroko/REUTERS; ORTN - Télé Sahel/AFP/Getty; Mikhail Metzel/TASS/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa mataifa hayo matatu Bakary Yaou Sangare wa Niger,  Abdoulaye Diop wa Mali na Karamoko Jean-Marie Traore wa Burkina Faso walikutana siku ya Ijumaa kukubaliana juu yamuungano huo wa ulinzi wa Mataifa ya Sahel AES.  

Eneo la Sahel limekuwa likikabiliwa na mashambulizi ya wapiganaji walio na itikadi kali kwa miaka kadhaa sasa na mataifa hayo matatu yameituhumu Ufaransa kushindwa kudhibiti hali.  

Ghana yamtaka Rais wa Senegal kusaidia kutatua mizozo ndani ya ECOWAS

Mwishoni mwa mwezi Januari mataifa hayo matatu ya Afrika, yanajiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, waliosema ipo chini ya ushwishi wa Ufaransa.