1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda yapitisha sheria kali ya kupinga ushoga

Bruce Amani
22 Machi 2023

Bunge nchini Uganda limepitisha sheria kali ya kupinga vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4P30x
Uganda führt drakonisches Anti-Schwulengesetz ein
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Muswada huo wa sheria unapendekeza adhabu mpya kali kwa wanaofanya mahusiano ya jinsia moja.

Serikali sasa itakuwa na mamlaka mapana ya kukabiliana na jamii ya wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTQ.

Muswada huo uliungwa mkono na wabunge wote 389 waliokuwa katika kikao cha jana isipokuwa mmoja tu.

Muswada huo sasa utawasilishwa kwa Rais Yoweri Museveni, kwa ajili ya kusainiwa kuwa sheria.

Chini ya sheria hiyo, yeyote anayeshiriki vitendo vya ushoga au anayejitambulisha kuwa mwanachama wa LGBTQ anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Katika miezi ya karibuni, uvumi kwamba kuna makundi ya kimataifa yanayokuza ushoga umesambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Uganda.