1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangladesh yakabiliwa na wimbi la joto kali

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Mamlaka nchini Bangladesh zimetoa tahadhari nyingine ya joto kali kwa siku tatu kuanzia Jumapili, wakati taifa hilo la kusini mwa Asia likikabiliwa na wimbi la joto kali kuwahi kushuhudiwa ndani ya kipindi cha miaka 75.

https://p.dw.com/p/4fGji
Bangladesch Dhaka | Wimbi la joto kali
Mkaazi wa Dhana akikabiliana na joto kali Picha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Mamlaka nchini Bangladesh zimetoa tahadhari nyingine ya joto kali kwa siku tatu kuanzia leo Jumapili, wakati taifa hilo la kusini mwa Asia likikabiliwa na wimbi la joto kali kuwahi kushuhudiwa ndani ya kipindi cha miaka 75.

Siku ya Ijumaa, nchi hiyo iliripoti kiwango cha juu cha nyuzi joto 42.7 katika kipimo cha Celcius katika wilaya ya kusini magharibi ya Chuadanga.

Ripoti: Mwaka 2024 unakaribia kuwa wenye joto zaidi kuwahi kutokea

Joto kali limeilazimu serikali kufunga shule kwa wiki nzima, huku hospitali zikijiandaa kupokea idadi kubwa ya wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi yatokanayo na joto kali, ikiwemo upungufu wa maji mwilini, uchovu na matatizo ya kupumua.

Wimbi la joto kali limedumu kwa siku 29 kufikia leo Jumapili, ikiwa ni kipindi kirefu tangu mamlaka nchimo humo zilipoanza kutunza rekodi za hali ya hewa.