1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia yawasilisha makubaliano ya amani kwa Arzebaijan

Lilian Mtono
16 Februari 2023

Armenia imewasilisha mpango wa makubaliano ya amani kwa hasimu wake Arzebaijan ili kumaliza mvutano uliodumu kwa miongo kadhaa juu ya jimbo la Nargono-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4NZnP
Armenien Türkei Grenze
Picha: Gilles Bader/dpa/MAXPPP/picture alliance

Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan ameliambia baraza la mawaziri kwamba jana Jumatano walikamilisha sehemu nyingine ya makubaliano hayo ya amani na yanayolenga kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia baina yao na Arzebaijan.

Soma pia:Azerbaijan yasitisha mazungumzo ya amani na Armenia

Tangazo hili linatolewa baada ya Armenia kuituhumu Arzebaijan kwa kutekeleza sera ya safishasafisha ya kikabila na kuwalazimisha watu wa kabila ya Armenia kuondoka kwenye jimbo hilo lililojitenga.

Mataifa hayo mawili yamepigana vita mara mbiliyakizozania udhibiti wa jimbo hilo la Azerbaijan lenye wakaazi wengi wa Armenia na kusababisha vifo vingi vya raia.